“If every day in the life of a school could be the last day but one, there would be little fault to find with it”BY Stephen Leacock.INGAWA SOMETIME ……………..............I MISS SCHOOL and old-new FRIENDS,siwezi kuwakutanisha tena isipokua hapa hapa
Friday, June 4, 2010
hivi ndivyo saidi alivyomuua mkuu wa mkoa wa IRINGA
Saidi alivyomuua(MURDER) mkuu wa mkoa wa IRINGA
Siku ya x-mas tarehe 25 mwezi wa kumi na mbili mnamo mwaka 1972 katika kijiji cha mkungigi katika mkoa wa iringa,bwana saidi mwamwindi alimuua mkuu wa mkoa wa iringa kwa kipindi hicho, kwakifupi tu saidi alikua dereva na akaamua kuachana na kazi hiyo mwaka 1954 nakuamua kuingia kijijini ndanindani kilometa 23 toka iringa mjini kuanza kufanya kilimo.
Akafanikiwa kuanzisha shamba lake kwa sheria za kimira kutoka kwa mkubwa wa kijiji ,saidi akaanza na eka 3 baada ya muda kidogo akamiliki eka 160 ,kipindi hicho pia na ujamaa pia ulikua ushaanza kuenea kwa kasi Iringa,
Siku moja kabla ya siku ya x-mas mkuu wamkoa alienda katika vijiji vya jirani kuwasaidia kuimalisha mashamba ya ujamaa lakini kutokana na mvua kubwa akufanikiwa kumaliza akawaahidi angerudi kesho yake,nandivyo alivyofanya kesho yake akaenda kipindi yupo njiani akamuona bwana saidi analima peke yake akamfwata na kumuuliza nani kampa kibali cha kutumia shamba peka yake ‘kwenye dunia ya ujamaa’
Akamjibu kuwa amepewa ruksa na wanakijiji wenzake, kutokana na maelezo ya kesi kwaupande wa mshtakiwa alisema mueshimiwa akaanza kumpiga piga na mkongojo kichwani huku akimtukana,kwa kuepusha shari akaamu kuondoka mueshimiwa akaanza kumfwata kwa nyuma akiendelea kumtusi.
Katikati ya njia akakuta mababuri akamuuliza saidi kwamba hii ni nini,saidi akajibu ni nyumba nilimowalaza ndugu zangu.mueshimiwa akamwambia kwamba ndimo walipolala xxxxxxxxx wenzako,
Saidi akapatwa na jazba akaingia ndani akachukua bunduki akampiga arafu akampakiza kwenye gari mpaka polisi na kuwakabidhi huku akijikabidhi………….mwisho wasiku akaukumiwa .
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment